Bei ya mafuta yapanda baada ya mashambulio dhidi ya vituo vya mafuta Saudia
at
September 16, 2019
Gharama ya mafuta imepanda kwa kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika miezi minne baada ya mashambulio mawili dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia Jumamosi yaliosababisha kumwagika kwa 5% ya mafuta duniani.
Kiwango cha mafuta ghafi yalipanda kwa 19% kwa thamani ya $71.95 kila mtungi huku viwango vingine, West Texas Intermediate, vikipanda 15% kwa thamani ya $63.34.
Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani. Huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya vituo hivyo Saudia kurudi katika hali ya kawaida. Mashambulio hayo dhidi ya vinu katika shina la viwanda vya mafuta saudia vinajumuisha kituo kikubwa duniani cha usafishaji mafuta.

0 comments: